HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2015

Lissu, Aponda Safari ya Matumaini ya Lowassa, adai ni ya ‘Matumizi’

Na Bryceson Mathias, Dodoma

MWANASIASA Machachari na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni,Tundu Lissu, ameponda Safari ya Matumaini ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, akidai si ya Matumaini, ni ya Matumizi.

Lissu alisema hayo katika Mkutano wa Hadhara alioufanya mkoani Dodoma jana katika Viwanja vya Barafu, ambapo pia alidai Watawala hao hawana uwezo tena wa kutawala kama kwanza.

Akiainisha Ishara za Watawala kushindwa kuongoza mbele ya Umati wa Wakazi wa    Dodoma, Lissu alisema kuwa ni pamoja na Migogoro na Migomo kila Kona, ambapo Wafanyabiashara, Madereva, Wanavyuo, Walimu, Wakulima na Wauguzi na Madaktari, safari hii waliiasi Serikali ya CCM.

Lissu ambaye alikuwa akihamasisha kujiandikisha katika Daftari la Kuduma la Kura, aliwakumbusha Wananchi akisema, mmewasikia wasaka Urais wa CCM wanaotoka Chama kimoja wanavyotofautiana kwa Kauli Mbiu, kila mmoja ana yake! Mkiona hayo, Ukombozi umefika.

“Lowassa amesema, ana Safari ya Matumaini; Safari hiyo si safari ya Matumaini ila ni Safari ya Matumizi, …Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba, amesema,  tutavushwa Ng’ambo, wengine acheni jamani…Watu wanasema, ‘Ukimwamsha aliyelala Utalala Mwenyewe”.alisema Lissu na wananchi wakshaangilia na kucheka.

Lissu alijinasifu akisema, Dhambi kubwa kuliko zote ambayo Watawala wa nchi hii wamewafanyia Watanzania, ni kuifanya nchi yetu kuwa Nchi ya watu Ombaomba, na ndiyo maana nimemsikia Mgombea Urais wa CCM, Makongoro Nyerere, akijinadi ‘tusiwape nchi hii Vibaka’.

Alisema, “Rais Jakaya Kikwete, anaomba, Mawaziri wake wanaomba, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi Wanaomba, Wakuu wa Mikoa wanaomba, Wakuu wa Wilaya wanaomba, na Polisi nao wanaomba!! Jambo hili ni aibu kwa Taifa.

Lissu alidai; Taifa hili limechafuka sana kwa Uovu ukiwemo, Wizi, Rushwa, Ufisadi na Mauaji ya Kutisha yanayomwaga Damu za Watanzania, hivyo linatakiwa kusafishwa… na njia pekee ni kujiandisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura, ili 25/10/2015, mtumie haki yenu.

Hata hivyo, Lissu alijigamba kwamba, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejipanga vizuri kuchukua Dola, na ndiyo maana walitoka nje wakipinga Katiba na inayopendekezwa na kura ya maoni, kwamba isingewezekana Aprili 30, sasa nani Mkweli?.alihoji.

No comments:

Post a Comment

Pages