HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2015

BONNY MWAITEGE KUZINDUA ALBAM TATU JUMAPILI





????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Uzinduzi wa albam ya muimbaji wa nyimbo za injili Bonny Mwaitege utakaofanyika jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, uzinduzi huo utashirikisha mwimbaji wa nyimbo za kutoka Zambia Ephraim Sekereti Faustine Munishi pia atashiriki kwenye uzinduzi huo na waimbaji wengine wengi kutoka hapa nchini
Fedha zitakazopatikana katika uzinduzi huo zitanunua baiskeli kwa ajili ya kuwapatia walemavu katika mikoa ya Ruvuma na Morogoro ambayo haikupata katika mgao wa kwanza na pia zitanunua Chakula kwa ajili ya vituo vya watoto yatima. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.


NA MWANDISHI WETU

UZINDUZI wa albamu tatu za mwimbaji nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Boniface Mwaitege, unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kesho huku asilimia kubwa ya maandalizi yakiwa yamekamilika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi huo, Alex Msama alisema maandalizi yote yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Msama mwasisi wa matukio ya muziki wa injili nchini tangu mwaka 2000, alisema jana kwao kama wadhamini, ni faraja kuona maandalizi yote yanakwenda vizuri na ametoa wito kwa wapendwa kujitokeza kwa wingi.

Msama, alizitaja albamu hizo kuwa ni pamoja na 'Tunapendwa na Mungu' yenye nyimbo za 'Tukiimba Mungu Anashuka', 'Mtoto wa Mwenzio ni Wako', 'Safari Bado', 'Tumekuja Kukuchukua (Bibi Harusi)', 'Tuko Salama', 'Moyo wa Shukrani', 'Hakuna Ridhiki' na 'Tunapendwa na Mungu' na albamu nyingine ni ‘Utanitambuaje’ na ‘Mama ni Mama,’ anasema.

Alisema uzinduzi huo uliodhaminiwa na kampuni yake, utashirikisha waimbaji mbalimbali maarufu wakiwemo John Lisu, Martha Mwaipaja, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Jesca BM, Ephraim Sekereti, Atosha Kisava, Mess Chengula, Upendo Kilahiro, Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe, Joshua Mlelwa na Anastazia Mukabwa.

Viingilio katika tamasha hilo kwa watoto watachangia sh 2,000 viti vya kawaida sh 5,000 na viti maalum sh 10,000.

Kuhusu waimbaji, Msama alisema wapo tayari kwa mashambulizi kwani nguli wa muziki wa Injili, Faustine Munishi anayefanya kazi zake nchini Kenya, ameshafika huku Ephraem Sekereti akitarajiwa kuwasili leo.




????????????????????????????????????

No comments:

Post a Comment

Pages