HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 28, 2015

Breaking News, Lowasa avunja ukimya, ajiunga rasmi na Chadema

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowasa (pichani) amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kutolizishwa na mchakato wa uteuzi wa wagombea wa urais uliomalizika wiki mbili zilizopita mkoani Dodoma.

Mh. Lowasa aliyefuatana na familia yake huku akiambatana na mke wake Regina Lowasa ambapo walikabidhiwa kadi za Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.  
 
Viongozi wa Ukawa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa NLD, Emmanue Makaidi, 

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba alisema kuwa endapo wataingia madarakani sheria pamoja na miswada mibovu iliyopitishwa bunge ikiwemo sheria ya mafuta na gesi watazifuta na kutunga sheria mpya kwa manufaa ya taifa. 

Aidha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alilitaka kundi la Frands of Lowasa kujiunga na Chadema ili kuongeza nguvu katika harakati za kuing'oa CCM madarakani.

 Wakazi wa jijini la Dar es Salaam wakiwa katika Bar ya Break Point wakifuatilia mkutano wa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Lowasa wakati akitangaza kujiunga na Chadema.
  Wakazi wa jijini la Dar es Salaam wakiwa katika Bar ya Break Point wakifuatilia mkutano wa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Lowasa wakati akitangaza kujiunga na Chadema.
 Vibanda vya wafanyabiashara vilijaa watu waliokuwa wasikiliza hotuba ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa wakati alipotangaza kujiunga rasmi na Chadema.
Watu wakifuatilia katika matangazo ya Televisheni.
 Umati wa watu ukifuatilia matangazo ya televisheni.

No comments:

Post a Comment

Pages