HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2015

CBA YAIBUKA BINGWA MASHINDANO YA SOKA YA MABENKI NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

 Baadhi ya wafanyakaz wa CBA Tanzania na Mkombozi wakishangilia uhamasisha timu zao uwanjani.
Mkurugenzi wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa  mechi ya fainali baina ya timu iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA imenyakua ubingwa
 Mkurugenzi wa CBA Tanzania Julius Mcharo akiongea na wachezaji baada ya kumalizika mchezo huo
 Wacheaji wa CBA Tanzania na Mkombozi wakiwa wamejipanga kukaguliwa kabla ya mchezo kuanza
 Wacheji wakionyeshana ubae uwanjani.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya soka ya Benki ya CBA Tanzania  imeichapa timu ya Benki ya Mkombozi FC kwa magoli 3-2 na kufanikiwa kuondoka na kombe la ligi ya mabenki na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mwaka huu sambamba na kitita cha shilingi milioni moja taslimu katika fainali zilizofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Vinara wa mabao waliong’ara katika mchezo huo ni Jessy Nyambo wa CBA FC David wasongwa wa Mkombozi FC.


Pia timu ya Benki ya Mkombozi ambayo iliibuka na ushindi wa pili ilijinyakulia kitita cha shilingi laki nane na kombe.


Akizungumza wakati wa fainali hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Dar es Salaam Emanuel Kazimoto,  alisema kuwa mashindano hayo ya taasisi ni muhimu kwa kuwa yanaziunganisha taasisi mbalimbali kuwa na ushirikiano katika kazi na wafanyakazi kuweza kujenga miili yao kupitia kufanya mazoezi na aliahidi kuwa watazidi kuunga mkono mashindano ya aina hii na kuzishauri taasisi hizo kubuni mashindano ya aina mbalimbali yatakayoshirikisha wafanyakazi wengi zaidi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,Julius Mcharo alisema amefurahishwa na ushindi ambao vijana wake wamepata na kuongeza kuwa wataendelea kushiriki na kudhamini michezo mbaimbali kwa kuwa  wanaamini kuwa michezo inaleta mshikamano na kujenga umoja ikiwemo pia kuimarisha afya.


Meneja Masoko wa Benki ya Mkombozi Grace Mboya,alipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano hayo na kusema kuwa kinachotakiwa ni kujiimarisha zaidi ili yazidi kuongezeka ubora kwa kushirikisha timu za taasisi zote zilizopo katika sekta ya fedha.

Baadhi ya wachezaji wa timu hizo ambao ni wafanyakazi wa enki hizo wamesema kuwa mashindano hayo yameweza kuwakutanisha na kuweza kufahamiana zaidi na pia ni moja ya mazoezi ya kujenga miili yao.Michuano hiyo iliyoanza Mwezi April 2015 na kufunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba yameshirikisha timu za soka za mabenki na mashirika ya hifadhi ya jamii.


Mkurugenzi wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa  mechi ya fainali baina ya timu iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA imenyakua ubingwa

No comments:

Post a Comment

Pages