HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2015

DC Mwanga awatoa hofu na kuwapongeza Wananchi

Na Bryceson Mathias, Kibindu Bagamoyo

KUFUTIA Kukamatwa na Kuuawa kwa Magaidi, ambapo jana Matatu yalidakwa na Polisi   na Silaha ya SMG, Risasi 50, Nondo Fupi 45 na Mabomu, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Madjid Hamad Mwanga, amekwenda eneo la Tukio kuwapongeza Wananchi kwa Ushirikiano na kuwatoa Hofu.

Mtendaji Kata Kata ya Kibindu, Godwini Mhagama, alipoulizwa na Mwandishi aliyekuwa mafichoni (Juu ya Mti) akiwa na baadhi ya Wananchi wnaofanya Ulinzi wa Kijadi, ajue hali ikoje Ki-Ulinzi na Ki-Usalama katika Kata yake  alisema, 

“Mwandishi; Mimi leo siko Kibindu nimesafari, Mpango wa Ulinzi upo palepale, na lakini leo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo (Mwanga), ataongea na Wananchi wa Vijiji vya Kibindu, na Pera kuliko na matukio ya Ugaidi ili kuwatoa Hofu juu ya Usalama wa Maisha na Mali zao, 

“Mkuu wa Wilaya anakwenda kuwahakikishia Wananchi kwamba, Serikali iko Imara, Kama wanavyoona ‘Juhudi za Jeshi la Polisi likiwakamata Magaidi hao kila wanapotoa Ushirikiano wa kutoa taarifa; Ndivyo Serikali ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa, itakavyofanya kuwalinda.

Mwandishi alipomtafuta Diwani wa Kata ya Kibindu, Mawazo Mkufya (CCM), aliyesaidia kuwanasa Magaidi Watatu (3) jana (alipokuwa kwenye Basi la Passion), mawasilino yake yalikuwa Mabovu, maana alikuwa kwenye Kelele za Maandalizi ya Mkutano wa Mkuu wa Wilaya.

“Mwandishi….Pole na Baridi ya Njeura; Tuna kwenye Maandalizi ya Mkutano na Mkuu wa Wilaya, anakusudia kuhutubia Waananchi wa Kibindu na Pera….ili kuwatoa hofu wananchi wafanye shughuli zao za Kiuchumi, maana hali imedhibitiwa”.alisema Mawazo….Simu ikakatika!.

Mapema asubuhi, Mtendaji wa Kijiji cha Kibindu, Juma Mhagama, alisema hali siyo mbaya kama ilivyokuwa siku zingine ambazo watu wamekuwa hawalali!...; Pamoja na kwamba bado Watu wana hofu ya kwenda mashambani kufanya shughuli zao za kila siku za kiuchumi…Leo ni shwali, inatia Moyo!..

Aidha Mwandishi alijaribu kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Bagamo (Mwanga) kwenye Simu yake [0784876158], ili asema japo neon…., simu yake iliita bila Majibu, na hadi tunaingia mitamboni, Mkuu wa Wilaya (Mwanga), hakuweza kufanya mawasiliano yoyote toka kwake, ila Kesho au Usiku, Mwandishi atajaribu kuwasiliana naye ili kuwahabarisha wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages