HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2015

Kigaila wa Chadema awabwaga washindani wake kura za maoni Dodoma Mjini

Na Bryvceson Mathias, Dodoma

MKURUGENZI wa Oganaizeisheni na Mafunzo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila, ameibuka Mshindi katika Kura ya Maoni ya Chama hicho, kugombea ubunge  wa Jimbo la Dodoma Mjini, baada ya kuwabwaga na kuwatupa mbali washindani wake .

Akitoa shukrani kwa wapiga kura Jana Kigala alisema, “Kazi yangu kubwa itakuwa kuhakikisha napambana na Rushwa, Ufisadi na Manyanyaso ya Ardhi, ambayo Wakazi wa Dodoma wanafanyiwa na Chama Tawala (CCM) na Serikali yake, hasa masuala ya ardhi”.alisema Kigala.

Katika kura za maoni Kigaila alipata kura 168, huku mpinzania wake, Joseph Kihoza, akiwa na kura 25 na aliyefuatia alikuwa na kura 4 na wengine walikuwa washindana kwa kufungana kwa Kura tatu tatu.

Mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo Mwl. Eneck Mhembano,  aliyewahi kuwa Mgombea wa Chadema wa Ubunge 2010 na kuwa mshindi wa pili aliwataka Chadema kushirikiana katika kufanya kazi ya kukijenga Chama, ili kuweza kuking’oa CCM.
 
“Wakati tunagombea Ubunge 2010, Kura za maoni hazikuwepo, walinifuata na kuniomba nigombee, Walinipa Katiba ya Chadema, nikaisoma vizuri, nikaielewa, nikaingia ulingoni na kupata kura nyingi nikawa Manukato dhidi ya Mgombea wa CCM.

“Kwa sasa chadema kimekua hadi tunafanya kura za maoni ili kumpata mgombea mmoja. Hivyo kati yetu humu ndani,  nasema ni lazima apatikane mshindi,  na mshindi huyo atakuwa chadema wala siyo mtu.”.alisema Mhembano.

Awali Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Jella Mambo, alisema, Chadema kina kazi kubwa moja tu, ni ya kuing’oa CCM madarakani,  ili kurejesha Imani kwa wananchi, kutokana na kushindwa kuwapatia Maisha Borakila Mtanzania iliyowaahidi, mbali na kukumbatia  Ruhwa, Wizi, Ufisadi, Watanzania wengi wakiendelea kuwa masikini.

No comments:

Post a Comment

Pages