HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2015

MAMIA WAJITOKEZA WAKATI LOWASSA AKICHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA

Ofisi za Makao Makuu ya Chadema zinavyoonekea zikiwa zimepambwa kwa bendera za chama hicho huku umati wa watu ukiwa nje ukimsubiri Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ambaye amejiunga na chama cha upinzani cha Chadema kuwasili kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chama hicho. (Picha zote na Francis Dande)
 Walinzi wa Chadema wakiwa katika maandalizi ya mapokezi ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa wakati wa zoezi la kuchukua fomu ya urais Makao Makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni Dar es Salaam.
 Wananchi wakimsubiri Edward Lowasa kuwasili.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakipekuliwa na maofisa usalama wa Chadema.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili Makao Makuu ya Chadema.
Mbowe akiwasalimia mamia ya watu waliojitokeza kushuhudia tukio laEdward Lowasa kuchukua fomu ya urais.
 Gari la Lowasa likiingia katika ofisi za Chadema.
Lowasa akiwasalimia wananchi waliojitokeza kushuhudia akichukua fomu ya kuwania urais.
Lowasa akiwapungua mkono mamia ya watu waliofika Makao Makuu ya Chadema wakati akichukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema.
Lowasa akiwasili katika Ofisi za Chadema.
Lowasa akiwa katikati ta umati wa watu wakati akiwasili katika ofisi za Chadema akiambatana na mke wake Regina.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifurahia jambo na Edward Lowasa.
 Edward Lowasa akiteta jambo na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lisu.
Edward Lowasa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lisu.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu ya urais mwanachama mpya wa chama hicho, Edward Lowasa. Kushoto ni Regina Lowasa.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi fomu ya urais mwanachama mpya wa chama hicho, Edward Lowasa.
Lowasa akiwaonyesha waandishi wa habari fomu ya urais baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Kushoto ni Regina Lowasa.
Mwanasheria wa Chadema Tundu Lisu akipeana mkono na Edward Lowasa.
Freeman Mbowe akiwa na Lowasa wakiwapungia wanachama na wapenzi wa Chadema waliofurika Makao Makuu ya Chadema.
 Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akitoka Makao Makuu ya Chadema baada ya kuchukua fomu ya urais.
Mama Regina Lowassa akitoka Makao Makuu ya Chadema.
 Lowassa akiwaaga wanachama na mashabiki wa Chadema baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema.

No comments:

Post a Comment

Pages