HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2015

ROBO FAINALI KAGAME KUANZA KESHO

Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuanza kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kwanza utakua ni kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan.

Saa 10:15 kamili jioni, Gor Mahia mabingwa wara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na Malakia kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo hiyo ya jumanne cha chini kitakua ni elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu kitakua ni elfu kumi na tano (15,000).

Robo fainali zitaendela siku ya jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira Afrika Mashariki yakielekezwa kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.

Kabla ya mechi hiyo ya wapinzani wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10 jioni, mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy kutoka nchini Sudan.

Viingilio vya mchezo wa siku ya jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilo cha juu kitanua ni elfu ishirini (20,000).

Katika hatua hiyo ya robo fainali endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare, hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).

CECAFA YAIPA ONYO GOR MAHIA
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiandika barua ya onyo klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza.

Katika barua hiyo ya CECAFA kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha kocha wake Frank Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na kanunu zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.

Kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa CECAFA juu ya tabia ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor Mahia, na kitendco cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.


ZUNGU AZINDUA AIRTEL RISING STAR
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu leo amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dare salaam, ambapo timu kutoka wiliya za Ilala, Temeke na Kinondoni zinashikriki michuano hiyo.

Akifungua michuano hiyo, Zungu amewatka vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya Airtel Rising kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika timu kubwa na kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.

Michuano ya Airtel Rising Stars imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka na kuibuka vipaji vya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji wenye vipaji huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka na wengine huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti U17).


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment

Pages