HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2015

SIMBA YAZINDUA KADI MPYA ZA KI-ELKTRONIKI KWA WANACHAMA WAKE

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii  kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita  hapa  kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.

Aliongeza  kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz . 

Napenda mtambue hii ni historia katika  ukanda huu kuweza kutumia  teknojia kufikia wanachama, Sisi  ni wakisa  sana  tunaona  mbele!.


Kwa  upande wake Afisa Mtendaji  Mkuu  wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati  ya masoko na  biashara Imani  Kajula  alisema.

‘Uanzishwaji  wa  Kadi  ya  Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa  kuwamemba  wa  Simba, bali  pia  kupata  punguzo   kubwa au kuingia  bure  kwenye  matukio  yanayo  andaliwa  na  Simba Sports Club. Pia  maduka  mbalimbali  yatatoa  punguzo  kwa  watoto  wenye  Simba Cub Card.

Wote  mna  jua fika  kuwa  mapenzi   hujengwa, Simb  aina lenga kujenga msingi  imara  wa kuendeleza  wanachama  na  wapenzi wake’’.
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za ki-elektroniki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa kibiashara na klabu hiyo na Makamu wa Rais, Geofrey Nyange Kaburu. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa kibiashara na klabu ya Simba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi hizo. 
 Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa kibiashara na klabu hiyo (kushoto) na Makamu wa Rais, Geofrey Nyange Kaburu wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za ki-elektroniki. 
 Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akimkabidhi kadi ya uanachama wa Simba mtoto Terrence Peter wakati wa uzinduzi wa kadi mpya za kielektroniki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula, ambaye kampuni yake ni washirika wa kibiashara na klabu hiyo.
Mussa Kova akipokea kadi yake mpya ya Ki-elektroniki kutoka kwa Rais wa Simba, Evans Aveva.
Viongozi wa Simba Evams Aveva (katikati) na Geofrey Nyange Kaburu pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula wakionyesha mfano wa kadi mpya za watoto chini ya miaka 18.
Watoto waliokabidhiwa kadi zao leo wakionyesha kadi walizokabidhiwa na uongozi wa Simba.
Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Simba baada ya kukabidhiwa kazi zao za kielektroniki.

No comments:

Post a Comment

Pages