HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2015

UMITASHUMTA na Changamoto zake

Meneja mauzo wa Isere Sports, Rasul Ndee akionesha aina ya mipira inayofaa kuchezewa katikaviwanja mbalimbali hapa nchini. (Picha na Mpiga Picha Wetu)
 Mkurugenzi wa Masoko wa Isere, Abbas Ally akionesha ainaya viatu vinavyofaa katika viwanja mbalimbali nchini (Picha na Mpiga Picha Wetu) 

Na Mwandishi Wetu


MASHINDANO ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) umeamalizika mjini Mwanza huku ikiacha changamoto kwa Serikali kushirikisha wadau kufufua na kuendeleza vipaji.


Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally ambao ni wauzaji wa vifaa michezo nchini aliyekuwa shuhuda wa michezo hiyo Mwanza alisema Tanzania imejaa vijana wenye vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa.


Alisema mikoa mingi imetia fora katika michezo hiyo ikiwemo mkoa wa Manyara,Singida na Mara ambako kujitokeza vijana wengi kupenda mchezo wa riadha na walifanya vizuri katika michezo hiyo.


Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally alisema mikoa mingi ilijiandaa kwa mashindano hayo lakini kuna tatizo la waamuzi ambao walionesha upendeleo kwa timu za Kanda ya Ziwa.


Alkisema mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa medali  26 ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka baada ya kupachikwa bao 1-0 na wenyeji Mwanza.


Ofisa Michezo Mkoa wa Morogoro, Neema Msita alisema kama vipaji vilivyoneshwa katika michezo ya mwaka huu vitaendelezwa Tanzania itarudisha heshima katika michezo kimataifa.


Alisema alitoa witokwa klabu zote kuanzisha timu za watotoambazozitalea vipaji kutokahatuaya shule za msingi, Sekondari na Vyuoni kwa vile Tanzania imejaliwakuwa na vipaji katika michezo yote.


Mtangazaji wa TBC Taifa, Jesse John aliyeshuhudiaufungaji wa mashindanohayo alisema kama kauli ya Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa ya kuwa wizara yake itasaidiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ukuzaji wa elimu sambamba na michezo utafanyiwa kazi hakuna timu ya taifa yaTanzania itakayotolewa katika mashindano kirahisi.

No comments:

Post a Comment

Pages