HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2015

Chadema msitumike kuchafuana

Na Bryceson Mathias, Mvomero

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mvomero, Ramadhani Mrisho, amewataka washindi wa kura za maoni ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa na kauli njema kwa wanachama wao ili kuepuka mamluki wanaotumika kuwachafua.

Mrisho alisema hayo kufuatia kuwepo taarifa za wanachama, kutumika na watia nia walioshindwa katika kinyang’anyiro cha udiwani na ubunge  katika kata na majimbo yao, wanaowashawishi wachovu wa siasa wawashitaki washindi wa udiwani na ubunge kwa uzushi.

Mrisho alisema amesikitishwa na baadhi ya wanachama na viongozi, ambao wanatumiwa na wapinzani wa Chadema, wanaotumia muda wao mwingi kutunga habari za uzushi kwa wanasiasa walioshinda kwenye kata na majimbo ya Chadema kwa lengo la kuwachafua ili Oktoba 25, maadui wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) washinde.

Mrisho alisema kuwa wapo watu ambao wanakosa sera za kisiasa na kuamua kuwachafua watu wengine kwa kuwapakazia mambo ambayo hayana kichwa wala miguu, hivyo Chadema Wilaya ya Mvomero ikiwabaini itawafukuza kwa kufuta taratibu za chama.

Akizungumzia suala la kujiunga kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, katika Chadema, alisema ni dalili nzuri ambazo zinaonyesha CCM imechoka na inatakiwa iondolewe madarakani kwa njia ya kidemokrasia bila kumwaga damu.

Amesema kutokana na hofu ya viongozi wa CCM kuanza kutengeneza mikakati ya kutaka kuwadhoofisha Watanzania wapenda maendeleo kwa kutunga uongo wakiwatumia Wana Chadema dhaifu, alidai kwa sasa wapo viongozi makini ndani ya Chadema.

“Watanzania naomba msisikilize maneno ya wazushi ambao wameishiwa sera, hakuna kiongozi makini ambaye anaweza kuondoka Chadema, tunapambana na adui ambaye ni CCM na ni lazima tumshinde tena kwa kishindo kikubwa,” alisema Mrisho.

No comments:

Post a Comment

Pages