HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2015

LOWASSA ATEMBELEA MASOKO YA CHAKULA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mgombea wa Urais kuoitia Ukawa, Edward Lowassa akiangalia maharage katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, leo wakati wa ziara take ya kuangalia hali ya masoko ya jijini Dar es Salaam.
Askari Polisi wakifanya mahojiano na dereva wa gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mgombea urais wa UKAWA kupitia Chadema alipotembelea masoko ya jiji la Dar es Salaam.

 Askari wa doria wakiwa wamezuia msafara wa Edward Lowassa baada ya kuvamiwa na waendesha bodaboda.
 Mgombea wa Urais wa Ukawa akinunua maji ya kandoro katika eneo la soko la Tandika jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea masoko ya chakula jijini Dar es Salaam.
Mgombea Mwenza wa Ukawa, Duni Haji Duni akiwapungia mkono wakazi wa Tandika.
 Lowassa akihojiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Lucas Mkondya.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Lucas Mkondya.
 Lowassa akipita katika soko la mitumba Tandika.
Lowassa akipata maelezo katika soko la samaki la Tandika Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages