HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2015

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA KITAIFA YA NANENANE LINDI

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inashiriki kwenye maonesho ya Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Katika maonesho hayo ambayo yanabebwa na Kauli Mbiu ya Matokeo Makubwa Sasa: Tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya  kilimo na ufugaji, NSSF itakuwa ikitoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu juu ya scheme zake za Wakulima na Wavuvi, kuandikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango  na kutoa elimu ya mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF kama vile matibabu, kuumia kazini, uzazi, pensheni ya uzee,ulemavu na urithi.

Kauli mbiu ya mwaka huu inaendana sana na azma ya NSSF kuwafikia wakulima,wafugaji na watu wengine wasio katika ajira rasmi kujiunga na mfuko huo na kupata mafao yote saba sawa na walio katika ajira rasmi.Aidha Shirika limeshaandikisha wanachama zaidi ya elfu sabini kutoka katika sekta isiyo rasmi na malengo ni kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.
NSSF inawakaribisha wakazi wa Lindi na Mtwara kwenye Banda lao ili waweze kupata huduma hizi kwa ajili ya kuboresha maisha yao na familia zao.
 Banda la NSSF linavyoonekana kwa mbele kwenye Maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi.

 Kaimu Meneja wa Mkoa wa Lindi, Deo Kabogi (kulia), akimpa maelezo mwanachama juu ya mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF wakati Ofisa Uandikishaji,  Tuli Mwaipopo akichukua taarifa za mwanachama mwengine kwa Lengo la Kumtengenezea kadi mpya ya NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi mwishoni mwa wiki.
Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi Kabonwa Kandoro akitoa maelezo kwa mmoja wa wanachama wa NSSF waliotembelea kwenye Banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro akimpa maelezo mmoja wa watu waliofika kwenye Banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi.
Afisa Teknohama, Rukia Penza akimpata taarifa za michango yake mmoja wa wanachama aliyetembelea kwenye Banda la NSSF.
Afisa Uandikishaji wa NSSF Mkoa wa Lindi Tuli Mwaipopo akichukua taarifa za Mwanachama kwa ajili ya kutengeneza kadi mpya ya mwanachama huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages