HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2015

SUMAYE AWASHANGAA WANAOVUMISHA KUIAMA CCM



WAZIRI Mkuu wa zamani Frederick Sumaye, ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kuvumisha kuwa angekutana na vyombo vya habari ili kujivua uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Siku za hivi karibuni tangu kuhama kwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Eduard Lowassa, kumezuka wimbi kubwa la baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kujivua uanachama na kuhamia Chadema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sumaye, alisema taarifa hiyo ilimshangaza kwa avile hakuwa na mpango huo.

Alisema hivyo kwa vile hakuwahi kuzungumza na mtu yeyeto na hajui chochote kuhusu mkutano huo na vyombo vya habari isitoshe hivi sasa yuko Hanang.

“Mimi watu ambao wameniuliza nimewambia yani hiyo kitu hata mimi sijui kiukweli wala siko Dar es Salaam.

“Ninasikia kuna mwandishi ameamua kutupia taarifa hiyo kwenye mambo yenu haya ajabu ajabu, hajazungumza na mimi wala sijawahi kuzungumza naye wala sina mpango huo,”alisema Sumaye.

Kuhusu kuhamia Chadema, Sumaye, alisema kama angehamia chama hicho angeviambia vyombo vya habari au angeonekana akipewa kadi.

“Hivi mimi naweza ni kamahama kisiri siri kweli ni waambi tu kuwa sina mpango wowote wa kukihama chama hiki,”alisema Sumaye.

Sumaye, aliwashangaa na haelewei wanaofanya hivyo wana lengo gani naye, akidai mbona hawaandiki taarifa za hao wanaohama, wange waandika hao kama wanataka kuandika.

No comments:

Post a Comment

Pages