HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 09, 2015

BOA yazindua huduma mpya ya Wari

Afisa Masoko wa Bank Of Africa (BOA), Daniel Sarungi akielezea huduma mpya ya Wari iliyozinduliwa na benki hiyo kwa ajili ya utumaji na upokeaji wa fedha kimataifa.
Mkuu wa ICT wa BOA, Bwana Willington Munyaga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma mpya ya Wari

Katikati ni Meneja huduma za Kielectronic wa BOA Editha Jumbe


Bank Of Afrika imezindua huduma mpya ya kutuma na kupokea fedha kutoka mahali popote duniani kwa gharama naafuu.

Kwa mujibu wa Afisa masoko wa Benki hiyo, Daniel Sarungu huduma hiyo itakuwa ikiwahudumia watu wote wenye akaunti kwenye benki hiyo pamoja na wale wasio na akaunti.

“Ni benki ambayo itawahudumia watu wote wenye akaunti hapa kwentu na wasio na akaunti,”alisema.

Mkuu wa ICT wa benki hiyo, Willington Munyaga aliwataka watanzania kuitumia huduma hiyo kwa madai kuwa ni njia salama na rahisi na kwamba, itakuwa ikitolewa katika matawi yote 21 ya benki hiyo yaliyo Dar es salaam nan je ya jiji la Dar es salaam.

Meneja wa huduma za kielectronic Editha Jumbe alisema kuwa, wateja wa huduma hiyo watakuwa wakipokea ujumbe wa simu mara wanapotuma fedha zao na wakati zinapotolewa na kuondoa gharama ya kupita simu au kutuma email hasa kwa wateja wa ughaibuni ili kujua kama wamepatiwa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages