HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 06, 2015

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITILIMA NJALU SILANGA AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI KIJIJI CHA ZANZUI

Mgombea ubunge jimbo la Itilima (Bariadi Mashariki), Njalu Silanga (CCM), akiwasili katika kijiji Zanzui Mlimani wakati wa mkutano wa kampeni. (Picha na Loveness Bernard)

Na Mwandishi wetu, Bariadi


Mgombea ubunge jimbo la itilima (Bariadi mashariki)Njalu Silanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amewaomba wananchi  kuchagua Chama hicho ili waweze kupata suluhisho la matatizo yao.


Njalu amesema hayo katika mikutano ya kampeni za kuomba kuchaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi huu nchini kote alipokuwa kata za Ndoleleji na Migato.


''Tunaomba mchague CCM kwani ndio Chama bora ambacho kinaweza kutatua shida zenu kwani wanazijua na wanaweza kuwatatulia kwani ilani yao ya uchaguzi imeelezea namna yakukabiliana na kutatua matatizo.


Aidha amewataka wananchi kutokujihusisha na vurugu zozote ambazo watashinikizwa na watu mbalimbali kwani wanaweza kuumia, kufungwa ama kuachwa na vilema vya maisha
Mgombea ubunge jimbo la Itilima (Bariadi Mashariki), Njalu Silanga (CCM), akimsalimia mtoto mdogo katika kijiji Zanzui Mlimani.
Mgombea ubunge CCM jimbo la Itilima (Bariadi Mashariki), Njalu Silanga akimsalimia mtoto mdogo katika kijiji Zanzui Mlimani.

No comments:

Post a Comment

Pages