Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jaji mstaafu, Damian Lubuva akitoa hotuba yake.
HOTUBA YA UFUNGUZI YA MWENYEKITI WA TUME YA
TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA NEW AFRICA
HOTEL TAREHE 12/10/2015.
Viongozi wa Vyama vya
Siasa,
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi,
Waheshimiwa Makamishna wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Inspekta Jenerali wa
Polisi,
Msajili wa Vyama vya
Siasa,
Viongozi wa Serikali,
Watendaji wa Mradi wa
Uimarishaji wa Demokrasia (DEP),
Watendaji wa Tume,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii
kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo
kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi
Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano
wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru
kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini
na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.
Viongozi wa Vyama vya
Siasa,
Pamoja
na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo katika kutekeleza
majukumu yenu kisiasa ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama
vya Siasa ni Wadau muhimu wa Uchaguzi ambapo mkishirikiana kutekeleza
majukumu yenu kwa
ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.
Viongozi wa Vyama vya
Siasa,
Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii,
Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu
kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa
yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii
nzima ya watanzania
Viongozi wa Vyama Vya
Siasa
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 64,736,
ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 156 na Zanzibar ni Vituo 1,580. Kila kituo
kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga
Kura 450 na wasiozidi 500. Hata hivyo
Kituo kinapokuwa na wapiga Kura zaidi ya
500 kinabidi kigawanywe ili viwe viwili yaani Kituo “A” na Kituo “B” na namba
ya Wapiga Kura itakuwa nusu kwa nusu.
Wapiga Kura wanashauriwa kwenda katika vituo walivyojiandikishia kupiga
kura siku nane (8) kabla ya siku ya
kupiga kura ili kuweza kujua Vituo vyao halisi vya kupigia kura.
Sambamba na hilo wananchi wataweza kupata
taarifa zao zilizoko kwenye kanzidata (Database) kwa kutumia simu zao za
kiganjani kupitia ujumbe mfupi wa maneno ‘sms’ bila wao kulazimika kufika
vituoni, namba hiyo ni *152*00# na kufuata maelekezo. Au kupitia Tovuti ya Tume
ambayo ni (www.nec.go.tz)
No comments:
Post a Comment