HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 04, 2015

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA YA BENKI YA CRDB

Mkurugenzi Mtendaji wa ki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni alipofika katika tawi la Azikiwe Premier wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kushoto ni Mkurugenzi wa tawi hilo, Fabiola Mussula. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akisubiri kuwahudumia wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiwahudumia wateja wa Benki ya CRDB waliofika kupata huduma katika tawi la Azikiwe Premier.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiwahudumia wateja wa Benki ya CRDB waliofika kupata huduma katika tawi la Azikiwe Premier.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiwahudumia wateja wa Benki ya CRDB waliofika kupata huduma katika tawi la Azikiwe Premier.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiwahudumia wateja wa Benki ya CRDB waliofika kupata huduma katika tawi la Azikiwe Premier.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakisubiri kuwahudumia wateja waliofika katika tawi la Azikiwe Premier.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakisubiri kuwahudumia wateja waliofika katika tawi la Azikiwe Premier.
Dk. Charles Kimei akiwsalimiana na wateja waliofika katika tawi la Azikiwe Premier.
Keki maalum kwa ajili ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akikata keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea katika matawi yote ya Benki hiyo. 
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula (Katikati) akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kukata keki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimlisha keki mteja wa benki hiyo.
Cheers kwa afya njema.
Mkurugenzi wa tawi la Premier, Fabiola Mussula akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi.
 Nyasigwa Mhagama akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mteja wa Benki ya CRDB, Rose Rimoi akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa benki hiyo, Kundasem Swai ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Azikiwe Premier jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa tawi la Premier, Fabiola Mussula. 
Mkurugenzi wa tawi la Premier, Fabiola Mussula (kushoto) akiwaongoza wafanyakazi wa Benki hiyo kufanya usafi katika Soko la Samaki la Feri.

Wafanyakzi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier wakifanya usafi katika Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussulu akimkabidhi vifaa vya kufanyia usafi Mkuu wa Soko la Samaki la Feri, Solomon Mushi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipofika sokoni hapo na kufanya usafi katika soko hilo, mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussulu akimkabidhi vifaa vya kufanyia usafi Mkuu wa Soko la Samaki la Feri, Solomon Mushi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo wafanyakazi wa benki hiyo walifanya usafi sokoni hapo. Kushoto ni Ofisa Afya, Dolah Minja.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussulu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa soko hilo pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la azikiwe wakiwa ndani ya ngarawa baada ya kufanya usafi katika Soko la Feri.
Ngarawa ikiingizwa baharini kwa ajili ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier kuanza safari ya kutalii katika bahari ya hindi eneo la Feri baada kushiriki zoezi la kufanya usafi katika soko hilo..

Ngarawa ikiingizwa baharini kwa ajili ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier kuanza safari ya kutalii katika bahari ya hindi eneo la Feri.

Nahodha akiweka sawa chombo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier wakiwa katika bahari ya hindi eneo la Feri.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier wakiwa katika bahari ya hindi eneo la Feri baada ya kufanya usafi katika soko la samaki.
Picha ya pamoja


NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kwa mwaka uliopita waliajiri watumishi 600 wa kada mbalimbali huku akijivunia ukuaji na ubora wa huduma za benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo tawi la Azikiwe Premier Dk. Kimei alisema ni fahari yake kuona benki hiyo ikiongozwa na watanzania.

Alisema maadhimisho ya wiki hiyo ni wakati wa kujipima kiutendaji na kuongeza ufanisi katika utuaji huduma ili kuifanya benki hiyo kuwa kinara wa huduma bora.

“Mwaka jana wakati wa wiki kama hii tulikua na kaulimbiu ilisema Asante, mwaka huu kaulimbiu inasema Asante Sana maana yake ni kwamba tumeongeza idadi ya wateja wanaofurahia huduma zetu,” alisema Dk. Kimei.

Rose Rimoi mkazi wa Mbezi Beach ni mteja wa benki hiyo katika tawi la Azikiwe Premier aliupongeza uongozi wa CRDB kwa kuboresha huduma zao na kuwajali wateja.

“Nahudumiwa na tawi hili kwa zaidi ya miaka minne sasa, huduma zinaboreshwa kila siku ndio maana hata wao wanaona ongezeko la wateja… nitaendelea kuweka fedha zangu hapa,” alisema Rose aliyepata zawadi kwa kuwa mteja wa kwanza kuhudumiwa.

Mkurugenzi wa tawi hilo, Fabiola Mussula aliahidi kuboresha huduma kwa wateja wake huku akieleza kuwa mikakati ya ofisi yake kwa wiki ya huduma kwa wateja ni kuwatembelea wateja wao.

“…Tutafanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kusafisha maeneo ya soko la kimataifa la samaki, feri pia kuanzia jumatatu hatutakaa ofisini, tutatoka, tutawafuata wateja wetu wadogo na wakubwa popote walipo,” alisema Fiola.

No comments:

Post a Comment

Pages