HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 27, 2015

MASASI YAFIKIWA NA KAMPENI YA NSSF KWANZA

Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara leo imekuwa miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Mtwara ambazo zimefikiwa na Kampeni ya NSSF Kwanza. 

Kampeni hii inayoendelea Tanzania Mzima kwa kuwafikia wakazi walio kwenye sekta binafsi kama vile Madereva wa Bodaboda, Wakulima, Wavuvi na wengineo.

Kampeni hiyo yenye lengo la kuelimisha umma juu ya faida za kujiunga na Mfuko wa NSSF, Kuhamasisha uandikishaji ili kupanua wigo wa wanachama na Kukusanya maoni ya mrejesho kutoka kwa wananchi ambao tayari ni wanachama juu ya huduma zitolewazo na NSSF ilianzia mikoa ya Kaskazini na inaendelea Mikoa ya Kusini.

NSSF inaendelea kuwasihi wakazi wa Mtwara waendelee kujiunga na NSSF ili wajipatie mafao bora.
Wakazi wa Masasi wakiwa wamejipanga mstari ili kujiunga na NSSF wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha watu walio kwenye sekta binafsi ili waweze kujiunga na NSSF na kujipatia mafao mbalimbali hasa ya Matibabu bure kwa wanachama na familia zao. Kampeni hii inaendela katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mtwara.
Afisa Uendeshaji mwandamizi Mkoa wa Mtwara, Yasin Kisawike akimwandikisha mkazi wa Wilaya ya Masasi kujiunga na NSSF baada ya kupatiwa maelezo kwenye kampeni maalum ijulikanayo kama NSSF Kwanza inayoendelea Mkoani Mtwara.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi Salim Kimaro (kulia) akihamasisha wakazi wa Masasi kujiandikisha na NSSF wakati wa kampeni maalum ya kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi ili waweze jiunga na NSSF kujipatia mafao mbalimbali ya NSSF yakiwemo kuumia kazini na Matibabu bure kwa wanaachama na familia zao.

No comments:

Post a Comment

Pages