HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2015

RAIS DK. MAGUFULI ALIHUTUBIA BUNGE

Rais Dk. John Magufuli akilihutubia bunge mjini Dododma wakati akilizindua bunge hilo. (Picha na Said Powa)
Marais Wastaafu, kutoka kushoto ni Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar,Amani Karume.
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiingia kwenye ukumbi wa bunge baada ya wapinzani kuanza kupiga kelele na kukaidi amri ya spika ya kukaa chini.
  Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiingia kwenye ukumbi wa bunge baada ya wapinzan kuanza kupiga kelele na kukaidi amri ya spika ya kukaa chini.
  Wabunge wa Upinzani wakiwa wamesimama na kupiga makelele wakikaidi amri ya spika kukaa chini baada ya Rais John Magufuli kuwasili ndani ya ukumbi wa bunge, huku wabunge wa CCM wakiwa wamekaa chini.
 Rais wa Zanzibar akiwaangalia wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakimzomea muda wote tangu alipoingia kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma. Kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi.
Wabunge wa upinzani wakitoka nnje ya ukumbi wa bunge baada ya kupinga kuwepo kwa rais wa Zanzibar ndani ya ukumbi huo, wakidai rais wa Zanzibar ni Maalim Seif.
 Wabunge wa upinzani wakitoka nnje ya ukumbi wa bunge baada ya kupinga kuwepo kwa rais wa Zanzibar ndani ya ukumbi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages