HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2015

UTT AMIS YATOA MSAADA KWA WATOTO NJITI


 Mhasibu Mwandamizi wa UTT AMIS Bwana Dogo Balima (kushoto) akimkabidhi Bi. Ruth Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa Ruth Mollel Foundation  hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia  watoto njiti.Kulia ni Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS Bw. Mfaume Kimario akishuhudia makabidhiano hayo.


 Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi Bw. Mfaume Kimario akiongea na waandishi wa habari baada ya UTT AMIS kutoa msaada kwa Ruth Mollel foundation kwa ajili ya kusaidia  watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Bi Ruth Mollel akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaaada ya shilingi Milioni 2 kutoka UTT AMIS kwa ajili ya kusaidia watoto njiti.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko  ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 250.

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns).  Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.

UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Pages