HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2016

AMSHA MAMA KUFANYIKA MWEMBEYANGA


NA LOVENESS BERNARD 
 
WATANZANIA wametakiwakujitokezakwawingikatikaTamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke jijini  Dar es Salaam .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi  wa Kampuni ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ilikuwapa fursa akina  mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi 

“ Akinamama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo  mbalimbali ikiwemo elimu” .AlisemaKariuki.

Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani  (Tundaman), amewaomba wakinamamawa changamkie fursa kwani watajifunza  mambo mengi

“Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini  kwaniniadimukutokea,” .alisemaTundaman.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .
Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim  ‘’Juma Nature’’,Khadija Kopa,Roma Mkatoliki,Young Killer,Msagasumu,Man fungo,Sharomwamba,Q-Chief,Mr
Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.

Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akina mama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.

Alisema  wamejipanga kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.

No comments:

Post a Comment

Pages