HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 04, 2016

Mwaitege wa kwanza Tamasha la Pasaka

NA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Bonny Mwaitege amekuwa wa kwanza kuthibitisha ushiriki wake katika Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 27 mwaka huu jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi huku wakifuatilia maombi ya mikoa mingine ambayo ina dhamira ya kufikiwa na Tamasha la Pasaka.
“Bonny Mwaitege ni mwimbaji wa kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka 2016 ambalo tumepanga kufanyika Mwanza, tumeridhika na maombi ya wakazi wa Mwanza ambao idadi kubwa ya maombi yao imeleta msukumo kwa Kamati kushawishika,” alisema Msama.
Naye Mwaitege aliishukuru na kuipongeza Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka kwa kumpa nafasi ya kwanza kuthibitisha kushiriki tamasha la mwaka huu, akisema Mungu ni wa kushukuriwa kwa sababu ni jambo jema ambalo linampa faraja kubwa.
Mwimbaji huyo alitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalumu, huku likihimiza upendo, amani na kudumisha ushirikiano kati ya waimbanji injili wa Tanzania na nchi jirani kama: Kenya, Rwanda, Zambia, Afrika Kusini na DR Congo.

No comments:

Post a Comment

Pages