HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2016

Ng'ombe 100 zadaiwa kukatwakatwa,Bonde la Mpunga Mgongola

Na Bryceson Mathias, Kigurukilo, Mvomero

NG'OMBE za Wafugaji ambazo bado hazinajulikana Idadi kutokana na vurugu inayotishia kutojua idai yake, zimekatwakatwa tena na wanaosadikiwa ni wafugaji katika Bonde la Mpunga Mngongola Kitongoji cha Kigulukilo, Kata ya Mkindo na Hembeti, Mvomero.

 Diwani wa Kata ya Hembeti, Peter Mdidi, amesema, haijulikani ni Ng'ombe wangapi wamekatwakatwa, lakini inasemekana wanaweza kufika 100 au zaidi.

"Tukio hilo lilianza juzi kati likisababishwa na na kilichoelezwa kwamba, tangu wiki iliyopita, wafugaji walikuwa wanalisha Ng'ombe mazao ya Wakulima kwa siri ukiwemo Mpunga, ambapo jana walikamata mifugo hiyo, kuafikiana kulipana kwa viongozi".alisema Mdidi.

Alisema wakati wakiwa katika maafikiano hayo, ghafla, wafugaji walitumia ujanja wa kutorosha mifugo hiyo, wakati polisi wakiarifiwa ili kutoa msaada, ambao Mdidi anasema, ulichelewa kuwafikia hadi walipofunga njia na kuzuia magari yaendayo Morogoro na Tanga (Mkindo Shortcut), wakidai afike Mkuu wa Wilaya, Betty Mkwassa!.

Mdidi amelilaumu Jeshi la Polisi kwa kusababisha Mzozo huo kuwa Mkubwa, ambapo alidai, alifanya kila jitihada ya kuwasiliana na OCD wa Mvomero, aliyesema yuko   Tanga, na alipomtaka msaada wa Mpelelezi wake alinyimwa ushirikiano hadi mambo yalipokuwa magumu, ikiidaiwa alikuwa kwenye tukio la Mauaji .

"Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima Mvomero na Kilosa, sasa umekuwa kama Mtaji kwa Viongozi wa Kisiasa na Vigogo wa Serikali na wilayani na mkoani, kutokana na kuwa wa figisufigisu za rushwa na ufisaji, huku wananchi wakipoteza maisha na mali zao'.alisema Mkulima mmoja, aliyetaka asitajwe!

Uongozi wa Ulinzi na Usalama wa wilaya ya Mvomero na Mkoa wa Morogoro, unajiandaa kwenda eneo la tukio wakiwa na vyombo vya Habari, Watu. Ng'ombe na mali vikiwa tayari vimeharibika! tayari kwa kutangzwa na kuonwa kwenye Runinga badala kufanya maamuzi magumu!

Mwaka jana Kijiji cha Dihinda, takrini Ng'ombe 150 waliuawa kwa kukatwakatwa Kijiji cha Dihinda, huku viongozi wa Kisiasa, Wakuu wa Wilaya, Mkoa, Wabunge na Mawazi, wakijigamba kukomesha na kuzuia wafugaji walioingiza mifugo waondolewe, lakini ilikuwa kama wimbo wa kurudiwa kwenye Kanda!,  

No comments:

Post a Comment

Pages