HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 28, 2016

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA SHINDA NA TemboCard KWA AJILI YA WATEJA WAKE

KIASI cha sh. bilioni moja kimetengwa kwa ajili ya zawadi mbalimbali kwa washindi wa kampeni ya matumizi ya tembokadi inayoendeshwa na Benki ya CRDB nchini kote.

Akizungumza leo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema lengo ni kuhamasisha matumizi ya kadi na kuepuka kubeba fedha nyingi.

Alisema kampeni hiyo ya miezi sita itatoa fursa kwa washindi 20 kila mwenzi huku mshindi wa kwanza kwa mwezi husika atapelekwa kwenye mbuga za wanyama pamoja na familia yake kwa siku tatu. “Nia yetu ni kuisaidia serikali kukusanya mapato ambapo kwa kutumia kadi yeyote ya CRDB mteja anaweza kulipia kodi ya mzingo, kulipa gharama za kuingia kwenye hifadhi za wanyama.

“Tunalenga pia kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya mtu kutembea na fedha nyingi ili kuepusha wizi, k
wa hiyo mshindi wa jumla baada ya miezi sita atapewa zawadi ya kwenda Afrika Kusini au Dubai pamoja na
familia yake kwa siku tatu,” alisema Dk. Kimei.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, hakuna malipo ya huduma kwa mteja anayetumia kadi za benki hiyo huku akibainisha kwamba zaidi ya watanzania milioni 1.6 wanamiliki kadi za CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei  akionyesha Tembo Card  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Shinda na TemboCard “ kwa ajili ya wateja wa benki hiyo, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay. (Picha na Francis Dande)
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei  akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu wa uzinduzi wa kampeni ya “Shinda na TemboCard “ kwa ajili ya wateja wa benki hiyo, Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay. 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay.
Ufafanuzi kwa waandishi wa habari. 
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi huo.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
 Tunasikiliza.

No comments:

Post a Comment

Pages