HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2016

HALMASHAURI TATU ZILIZOPATA HATI CHAFU

Na Malisa GJ

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;
1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)
Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. 

Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya Shs.178,511,580, Na walitumia Shs.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dk.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!
Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"
Na katika hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi.

 Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages