HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2016

RAIS MAGUFULI ATINGA BENKI YA CRDB TAWI LA HOLLAND

Na Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera.

Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya saa saa nne asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.

 Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari  na kuingia ndani ya benki hiyo.

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa awakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo ilibidi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwisha ingia.

Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile kwani baadhi ya wananchi kudai kuwa hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa Tex, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa walishtuka lakini mara walimuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana.
Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu, alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi nwakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,”alisema.


Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
 Rais John Magufuli akiwa ndani ya gari lenye namba za usajili T182 DFQ huku akiwapungia mkono watu waliokuwa nje ya  Benki ya  CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoka katika benki hiyo. (Picha na Francis Dande)
Muuza maji (kushoto) akishangaa gari alilopanda Rais Magufuli leo asubuhi wakati akitoka Benki ya CRDB tawi la Holland.

Gari alilokuwa amepanda Rais John Magufuli lenye namba za usaji T 182 DGQ likitoka katika benki ya CRDB tawi la Holland lililopo katika makutano ya barabara ya Samora na Ohio jijini Dar es Salaam.   

No comments:

Post a Comment

Pages