HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 03, 2016

56 WAFA KWA KIPINDUPINDU UNGUJA NA PEMBA

Na Talib Ussi, Zanzibar
Watu wapatao 56 wamefariki duni hadi juzi kutokana na kuenea Maradhi ya kipindupindu katika maeneo ya Unguja na Pemba.
Akizungumza  katika sikuku ya wafanyakazi ulimwenguni jana visiwani  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema ni hudhuni kubwa kuondokewan na watu kiasi hicho na kuwaomba wananchi kuwaangalifu maradhi hayo ya mripuko. 
“Inauma sana watu walikufa kutokana na kipindupindu ni wengi sanaa sisi ambao tupo hai tunatakiwa tufuate nasaha na mabwana Afya ili tuweze kuoko” alieleza Dk. Shein kwa masikitiko. 
Alisema kuwa watu 43 kati hao waliofariki ni kutoka kisiwa cha Unguja na 13 wanatoka kisiwa cha Pemba na kueleza na hali bado haijawa mzrui kwani bado kambi maalumu za maradhi hayo zimekuwa zikipokea wagonjwa wapya kila siku.
“Kambi yetu ya muda iliyopo Chumbuni wilaya Magharbi Unguja ina wagonjwa 56 ambayo kwa kweli bado hali ni mbaya lazime tukaze kamba kukabiliana nayo” alisema Rais huyo. 
Aliwaomba wananchi kuchemsha maji ya kunywa na kufuata marufuku ya serikali wakle wote ambao wanafanya biashara za vyakula. 
“Hatuna nia mbaya ya kupiga marufuku biashara za kula lakini jamanii hali ya maradhi ya kipindupindu ni mbaya sanaa” alieleza Dk. Shein.

Zaidi ya Wagonjwa 3448 wameugua ugonjwa huo tangu ulipoanza  Septemba 2015 kuwaacha wakazi wa miji mbali mbali visiwani hapa kuwa na hofu.

No comments:

Post a Comment

Pages