HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2016

Ligi Kuu Wanawake 'live' Azam Tv

·       TFF yasaini mkataba wa miaka mi5 na Azam Media Ltd

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo limesaini mikataba miwili na Kampuni ya Azam Media Ltd, ya Haki za Matangazo ya Televisheni ya michuano ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) na Ligi ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (U-20 National League).

Mikataba hiyo iliyosainiwa kwa mpigo, ina thamani ya Sh. Bil. 2, kwa kipindi cha miaka mitano, ambayo ilitiwa saini jana Makao Makuu ya Azam Media Ltd na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Malinzi alisema TFF inapenda kuishukuru Azam Media kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za shirikisho lake kunyanyua maendeleo ya soka Tanzania, kwa kuitikia maombi yao na kukubali kutoa udhamini.

Malinzi aliyataka makampuni mbalimbali nchini hasa yanayotoa huduma za kijamii zinazohusisha wanawake na watoto, kujitokeza kudhamini michuano hiyo, ambayo hadi sasa inapotarajiwa kuanza kuchezwa, haijapata Mdhamini Mkuu wa Mashindano.

Alibainisha kuwa, kutokana na Azam Media Ltd kuingia mkataba wa Haki za Matangazo kwa kipindi cha miaka mitano kuonyesha ligi hizo, kampuni na taasisi zingine zijitokeze na kuitumia fursa hiyo kama chachu ya kujitangaza kupitia udhamini wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages