HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 06, 2016

MTOTO WA KITANZANIA ASHIRIKI KATIKA FILAMU YA KIMAREKANI


Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.

Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.

Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7.

 Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi. 
Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake. 
Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony. 
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake. 
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.
Unaweza kuona clips za hiyo movie kupitia links hizi za youtube. 

Kwa walio Marekani na Canada, movie hiyo itaonyeshwa siku ya Ijumaa na Jmosi kupitia Lifetime Channel 8/7c

Tuendelee kumwombea mtanzania mwenzetu aende mbele zaidi ili tuzidi kuipeperusha bendera yetu. Evan amefanya audition nyingi kwahiyo Mungu akipenda ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu zaidi. 

Asante sana,

Dr. Philomena Ishengoma & Godfrey Byarushengo
Wazazi wa Evan

No comments:

Post a Comment

Pages