HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 21, 2016

SUKARI "YAKAUKA" MANISPAA YA KIGOMA-UJIJI

Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA
MKOA wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.
Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. “Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga
 Bandari ya Kigoma.

No comments:

Post a Comment

Pages