HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 27, 2016

LSA HIYOO YATIMKIA ARUSHA KUSHIRIKI ROLLINGSTONE ECAYFA 2016

  Wachezaji wa LSA wakiomba dua wakati wa michuano ya Rollingstone ilipofanyika jijini Dar.
  Nahodha wa LSA, Hamdani Sarahani akimkabidhi Mhariri wa Habari wa Tanzania Daima, Martin Malera, Kombe la LIMFA walilotwaa wakati walipotembelea ofisi za gazeti hilo
  Mkurugenzi na kocha wa LSA, Haffidh Karongo akitoa maelekezo kwa nyota wa kikosi chake wakati wa mapumziko ya moja ya mechi za Rollingstone.
Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba kushoto akiwa katika picha ya pamoja kikosi hicho.
NA MWANDISHI WETU 

MSAFARA wa wachezaji 22 na viongozi wawili wa timu ya Lindi Soccer Academy (LSA), umeondoka jijini Dar es Salaam leo Jumatatu asubuhi kuelekea Arusha, kushiriki michuano ya vijana kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ya Rollingstone (ECAYFA 2016). 

LSA yenye Makao Makuu mjini Lindi, iliondoka mjini humo jana Jumapili asubuhi na kuwasili jijini Dar es Salaam, kabla ya leo Jumatatu kuondoka kuelekea Arusha kushiriki ECAYFA 2016, inayoratibiwa na Akademi ya Rollingstone ya huko.

Michuano ya Rollingstone, ambayo inatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake na kujijengea heshima na umaarufu, mwaka huu inatarajia kuanza kesho Juni 29 hadi Julai 9, ikishirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 13, 16 na 20.

Akizungumza na HABARI MSETO, Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba, alisema kikosi chake mwaka huu kitashiriki michuano hiyo levo ya vijana chini ya miaka 16, ambako nyota wake wote 22 alionao safarini wanafuzu vigezo vya kucheza kategori hiyo.

Mkandemba alibainsiha kuwa, kikosi kiko kamili kila idara na kwamba wana matumaini makubwa ya kufanya vema, huku akizitaka taasisi, mashirika, kampuni na wadau wa soka kujitokeza kuisaidia timu yake ambayo inacheza mashindano hayo kwa mara ya pili.

Aliwataja nyota waliomo katika msafara huo kuwa ni Hamdani Sarahani 'Mido', Shaffih Maulid, Imani Chande, Lucas Julius, Masoud Kisige, Hassan Alubuni, Rajabu Saidi, Mukeshi Amani, Odio Victory, Mohammed Lijei na Banzalam Khamis.

Wengine waliotajwa na Mkandemba kuwamo safarini ni pamoja na Madulu David, Tuwa Saidi, Haji Mohammed, Mohammed Maneno, Ramadhani Bakari, Ramadhani Koyo, Peter Lucas, Farouq Karongo, Shazir Issa, Faraji Nurdin na Selemani Solomon.

No comments:

Post a Comment

Pages