HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2016

NAPE AONGOZA MAMIA KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA, JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faifa za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa, kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njiaya kupumua. Hali kadhalika unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Wazi Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya YogaDuniani kwenye ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
 Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati)
 Mkao wa mwili mfu kwa lugha ya Yoga, Savasana, mkao huu unasaidia kupunguza kila aina ya misukosuko na kutuliza mwili na akili.

 Waziri Nape katika mkao wa  "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika mkao wa  "Tadasana".
Mkao wa Pumzi Nyuki au kwa lugha ya Yoga, "Bhramari Pranayam", mkao huu una faida ya kupunguza msongo wa mawazo, na unasaidia kutoa wasiwasi, hofu, hasira na kuleta utulivu wa akili. Faida ya kutoa mlio kama wa Nyuki inasaidia kutuliza akili na mfumo wa neva, lakini pia ni mkao mzuri kwa kuleta utulivu kwa ujumla na kuepusha madhara ya msongo wa mawazo

No comments:

Post a Comment

Pages