HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2016

KAMATI YA MAADILI YA TFF KUKUTANA NA JERRY MURO

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  inatarajiwa kuwa na kikao chake Jumamosi Julai 2, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za TFF zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru, Ilala jijini Dar es Salaam.

Viongozi watatu kutoka wanachama wa TFF wanahitajika kufika kwenye kikao hicho kinachotarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi.


  1. Viongozi hao ni Jerry Muro - Msemaji wa Young Africans S.C
  2. Nassib Mabrouk - Katibu wa MZFA na Msimamizi msaidizi wa kituo cha Mwanza
  3. Mbasha Matutu - Mjumbe wa mkutano mkuu Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Pages