HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2016

NAPE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUPOKEA MWILI WA SENGA

Aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga enzi za uhai wake. (Picha zote na Francis Dande).
 Dada wa marehemu, Yunista Senga akisaidiwa na ndugu baada ya kuishiwa nguvu wakati wa kuupokea mwili wa marehemu Joseph Senga.
 Ndugu, Jamaa na Wafanyakazi wenzake marehemu Joseph Senga wakisubiri mwili Uwanja wa Ndege. 
 Mhariri wa Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo akipeana mkono na Waziri wa Habari, Sanaa, Tamaduni na Michezo, Nape Nnauye alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa kupokea mwili wa marehemu Joseph Senga.
Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa katika picha ya pamona wakati wakisubiri mwili wa marehemu, Joseph Senga.
 Mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti laTanzania Daima, marehemu Joseph Senga ukiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo ukitokea New Delhi India. 
Mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti laTanzania Daima, marehemu Joseph Senga ukiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leoukitokea New Delhi India. 
Baadhi ya ndugu na wafanyakazi wa Swissport wakibeba mwili wa marehemu. 
 Mwili wa marehemu ukiwa katika gari.
 Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa katika gari.
 Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Sanaa, Tamaduni na Michezo, Nape Nnauye. 
  Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga. 
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika kuupokea mwili wa marehemu wakitoka Uwanja wa Ndege.

Na Mwandishi Wetu

Mwili wa aliyekuwa mpigapicga wa mkuu wa gazei la Tanzania Daima marehemu Joseph Senga (58), umewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Julai 30 ukitokea New Delhi India.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena alisema shughuli za kuaga mwili wa marehemu zitaganyika saa tatu asubuhi nyumbani kwa marehemu maeneo Sinza White Inn.

Alisema baada ya kumalizikia kwa mchakato wa kuaga, marehemu atasafirishwa hadi mkoani Mwanza, wilaya ya Kwimba kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatatu.

Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Tamaduni na Michezo, Nape Nnauye alisema serikali itakuwa bega kwa bega na familia katika msiba huo. Alisema kifo cha Senga kimeacha simanzi nzito katika tasnia ya habari pamoja na wizara.

"Tasnia imempoteza mtu muhimu, hivyo hatuja jinsi zaidi ya kumuombea, lakini pia serikali inaungana katika wakati huu mgumu, "alisema Nnauye.

Naye mbunge wa Sumve, Richard Ndassa alisema kifo cha Senga ni pigo katika tasnia ya habari kutokana mchango wake. "Si habari tu hata jamii pia kwani kazi aliyoifanya ni ishara tosha kwamba ametuachia pengo, " alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages