HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 28, 2016

JWTZ YAKABIDHI VIKOMBE KWA MKUU WA MAJESHI

Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
 
Timu teule za Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania zilizowakilisha nchi katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki zimekabidhi kwa bendera na Vikombe ilivyonyakua wakati wa mashindano yaliyofanyika Kigali nchini Rwanda.
 
Akipokea Bendera na  Vikombe kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi ya ulinzi Brigedia Jenerali Alfred Kapinga alisema ushindi uliopatika ni faraja kwa watanazania na jeshi hivyo ni vyema kwa wanamichezo kujipongeza hasa ukizingatia ushindani mkubwa.
 
“Ushindi ni Ushindi hivyo hakuna budi kujipongeza kwa kuwa washindi kwani  vikombe vitat u vilivyopatika ni faraja na hasa kikombe cha Mpira wa pete ambacho tulikipoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda”,Alisema Brigedia kapinga.
 
Pia alizitaka Timu kuanza maandalizi kwa ajili ya mashindano yajayo lakini pia kujiweka sawa kwa mashindano yatakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kuibuka na ushindi zaidi ya ilivyokuwa sasa.
Aliongeza kuwa hakika jeshi limeamua kurejesha heshima yake kama ambavyo mkuu wa majeshi aliagiza katika michuano hiyo.
 
Pia aliwapongeza waandishi wa habari wa kushirikiana na JWTZ na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwani JWTZ ni timu ya Ushindi hivyo nao ni washindi na vivyo hivyo kwa wadhamini ambao amewaomba kuendeleza ushirikiano wao katika kuchangia mafanikio ya michezo kwa jeshi.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa michezo kutoka makao makuu ya JWTZ Brigedia Jenerali martin Busungu ameshukuru kwa ushirikiano na kuwapongeza wote waliofanikisha ushiriki wa JWTZ katika mashindano hayo na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
 
Alisema katika mashindano hayo waliyoshiriki michezo mitano ambAYO NI Riadha mpira wa Miguu, mpira wa pete ,mpira wa mikono na  mpira wa kikapu ambapo katika mpiwa wa miguu JWTZ imeshika nafasi ya tatu, Riadha Wanawwake nafasi ya tatu na Mpira wa pete nafasi ya kwanza na mchezaji Bora ambaye alikuwa na Nasra Suleiman.
 
Mbali na zoezi la kukabidhi vikombe pia bendera iliyokabidhiwa kwa wanamichezo hao imerejeshwa kuashiriia mwisho wa jukumu hilo walilokabidhiwa la kupeperusha vyema bendera ya taifa

No comments:

Post a Comment

Pages