HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 28, 2016

MISA TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA MWAKA 2016 KWA KUZINDUA CHAPISHO NA KUTOA TUZO

Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumzia vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.

MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. Hapa ni ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari kutoka UNESCO, Christopher Regay akichangia mada.
Meneja Viwango na Udhibiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Club ya Waandishi wa Habari mkoa wa Singida, Ranko Banadi akichangia mada 
Mwenyekiti wa Tanga Press Club, Hassan Hashimu akizungumza jambo wakati wa utoaji wa tuzo za utoaji wa taarifa kwa umma zilizotolewa na MISA Tanzania .
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Chapisho la upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma. 
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer( wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa( wa pili kutoka kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa taasisi za umma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer(katikati) akimpongeza Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao Makuu, Gabriel Mwangosi baada ya TRA kuibuka washindi wa kwanza katika utoaji wa habari kwa umma.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa.
Baadhi ya viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.

No comments:

Post a Comment

Pages