HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2016

WAANDISHI WA HABARAI WAASWA KUUSOMA MUSWADA WA HABARI

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga  akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016. Kulia ni Mwanasheria wa Sahara Media, Neriah Martin na Katibu wa TEF, Neville Meena.  (Picha na Francis Dande)

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

BAADA ya muswada wa Sheria ya habari kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni mwaka huu, wadau  wa habari wamewaasa waandishi wa habari nchini kuusoma na kuuelewa kwa ajili ya kutoa maoni yao.

Muswaada huo, ni ule uliyosomwa bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, na Michezo, Nape Nnauye, Septemba 16 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam Jana, kwa niaba ya Wadau wa Habari, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, alisema wadau hao wamekuwa wakipokea with katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo vya ndani na nje ya nchi, kuzungumzia au kutoa maoni kuhusu maudhui ya muswada huo.

"Wadau wanaoshiriki katika mchakato huo ni hawa, TEF, Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Umoja wa kudai Sheria za Haki ya Kupata Taarifa (CORI),"aliwataja Makunga.

Alisema maoni yao pamoja na wadaau wa habari yatawezesha  utunzi wa Sheria bora kwa masilahi ya nchi, sekta ya habari na taifa kwa ujumla, kwani sheria inayotumika sasa ni ya mwaka 1976 ambayo inalalamikiwa kuwa na upungufu mkubwa.

Aidha, Makunga, alisema wadau hao pia wameweka mpango utakaowezesha kukusanya maoni ya watu wengine kutoka mbalimbali nchini na yatakusanywa kupitia Klabu za Waandishi wa Habari ambazo zimesambaa nchi nzima.

"Muswada huu siyo mali ya wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri au vyumba vya Habari vilivyopo jijini Dar es Salaam pekee, bali unagusa masilahi mapana ya sekta nzima ya habari nchini.

"Sheria inayokusudiwa kutungwa inaweza kutumika miaka 50 ijayo au zaidi, kama ilivyo kwa Sheria ya Magazeti ya 1976 ambayo imekuwapo kwa miaka 40 sasa,"alisema.

Katibu wa TEF, Neville Meena, ambaye pia ni Mhariri Myendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, alisema ni wakati sasa kwa waandishi wa habari kuusoma muswaada huo ambao umeandaliwa kwa lugha mbili yani Kiswahili na Kingereza huku akibainisha kuwa muswaada huo unapatika kwenye mtandao wa Bunge.

Alisema kwa kuwa waandishi wa habari wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu kwa hiyo ni vema wakatumia fursa hiyo iliyojitokeza na kutoa maoni yao ambayo yanawakera katika Sheria iliyopo sasa.

Meena, alisema kabla ya kuhoji wandishi wa habari wanatakiwa kuanzisha mijadala hiyo ya upatikanaji wa maoni hayo bila kufikiria matokeo kwanza.

Aliongeza kwa kusema maoni naatakwa yao katika ushauri watakaoutoa kwa serikali kwa maana ya Wizara yenye dhamana ya kusimamia sekta ya Habari na Bunge ambalo ndilo lenye wajibu wa kutunga Sheria.

No comments:

Post a Comment

Pages