HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2016

DK. MGWATU AWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA KARAKANA ZA TEMESA

Mkuu wa Karakana ya Magari Chuo cha Ufundi Arusha Bw. Joseph Kotini (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu juu ya mtambo unaotumika kufanya ukaguzi na matengenezo makubwa ya magari chuoni hapo. (Picha na Theresia Mwami-TEMESA, Arusha).


Na Theresia Mwami, Arusha.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu ameahidi kuziimarisha karakana zilizopo chini ya TEMESA ili kuimarisha utendaji kazi.

Mikakati hiyo imetolewa leo na Mtendaji huyo alipokutana na watumishi TEMESA wa mkoani Arusha alipotembela kituo hicho kuangalia utendaji kazi wa kituo hicho.
“Naahidi kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe wafuatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufuatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu. 

Ameongeza kuwa amepanga mikakati namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na utunzaji wa taarifa zake, kufanikisha utendaji kazi wa baadhi ya karakana,kuwezesha urahisi wa  mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na vituo mikoani. 

Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake kuwa wanafanya kazi kwa mazoea, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.

Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu ametembelea Chuo cha Ufundi Arusha ili kujionea shughuli mbalimbali za mafunzo yanayotolewa chuoni hapo na amefurahishwa na vifaa vya kisasa vya kutengenezea magari vinavyotumika katika karakana ya chuo hicho kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wake.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Richard Masika alionesha nia ya kushirikiana kwa ukaribu na TEMESA ili kuweza kuboresha mafunzo ili kupata huduma zinazotolewa katika karakana za TEMESA.

Dkt. Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA Kanda ya Kaskazini ili kujionea changamoto na hali halisi ya utendaji kazi wa vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages