HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2016

UNIVERSITIES ABROAD YADHAMINI WANAFUNZI 220 NJE YA NCHI

SEHEMU ya tatu ya Wanafunzi 220 waliochaguliwa kusoma kwa Scholarship nje ya Nchi chini ya udhamini wa Universities Abroad wameondoka kwenda Nchini China na Uingereza.

Wanafunzi hao 35 wengi wao wakiwa kwenye fani ya Udaktari, Uhandisi na Biashara za Kimataifa watalipa ada ya mwaka mmoja tu wa kozi na wengine wakigharamia asilimia 50 ya gharama zote.

Taasisi ya UAL inaendelea na udahili kwa wanafunzi watakaokwenda Novemba na Februari 2017 katika ofisi zao zilizopo Posta Mpya jengo la  Benjamini Mkapa Tower na Ofisi ya Kanda- Mwanza, Kenyatta Road na Exim Bank Ghorofa ya pili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaaga wanafunzi 220 waliopata udhamini  wa masomo kutoka Universities Abroad Link. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), akizungumza na Esnath Mwaka (kushoto), ambaye ni mmoja wa wanafunzi 220 waliopata udhamini  wa Universities Abroad Link kwenda kusomea masomo ya Uchumi na Biashara za Kimataifa nchini China. Hafla ya kuwaaga ilifanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni David Mwaka. 
 Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda katika masomo nchini UK na China wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Universities Abroad Link muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kuelekea China na Uingereza katika masomo yao.
 Wanafunzi waliopata ufadhili wa Universities Abroad Link wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, walezi wao wakati wa kuwaaga Uwanja wa Ndege.
 Picha ya pamoja.
 Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwakilishi wa wanafunzi wanaokwenda China na Uingereza akitoa neno la shukrani muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kuelekea China na UK.

No comments:

Post a Comment

Pages