HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2016

ACT WAZALENDO YAJIPANGA UCHAGUZI WA MARUDIO JIMBO LA DIMANI-ZANZIBAR

Tunapenda kuwafahamisha wanachama wa ACT Wazalendo na umma wa watanzania kwa ujumla, kuwa kampeni  kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania bara ambazo chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi disemba 31/2016.

Kwa upande wa udiwani chama kilisimamisha wagombea saba na waliopitishwa na Tume ya uchaguzi ni wagombea sita baada ya mgombea wa kata ya Misugusugu mkoani Pwani kuenguliwa kugombea kutokana na pingamizi alilowekewa.

Kata ambazo chama cha ACT Wazalendo imesimamisha wagombea ni pamoja na   Isagahe,iliyopo Kahama mkoani Shinyanga,Kijichi, iliyopo Temeke jijini Dar esSalaam,Nkome iliyopo Mkoani Geita,Tanga iliyopo mkoani Ruvuma na Ihumwa iliyopo mkoani Dodoma.

Chama cha ACT wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa Taifa letu.

Pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli tunawaomba wahakikishe wanamchagua  mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo.

Tunawahimiza wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM  kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao
Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT Wazalendo
27/12/2016

No comments:

Post a Comment

Pages