HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2016

Askofu Kinyunyu; Tumelisha wafungwa wote Gereza la Isanga-Krismas

Na Bryceson Mathias Isanga, Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amoni Kinyunyu, amesema (KKKT) katika kuadhimisha Sherehe za Krismas ya 2016 kuelekea mwaka mpya  2017, imetumia Kilo 190 za Nyama, na Kilo 150 za Mchele kuwalisha Wafungwa wote wa Kike na wa Kiune wa Gerzeza la Isanga Dodoma.

Hayo yamesemwa na Askofu Kinyunyu mwishoni mwa wiki ambapo amesema Vyakula hivyo ambavyo vinagharimu zaidi ya Mil.1.5/-, vimetolewa na mmoja wa Wakristo wa KKKT Kanisa Kuu, Jimbo la Makao Makuu ambaye hakutaka atajwe jina lake akidai Mungu anamfahamu hivyo hapendi atajwe jina lake gazetini ila Askofu anamfahamu.

Akipokea Msaada huo, Mkuu wa Gereza la Isanga, Keneth Elia Mwambije, alisema, “Heshima hii na Utukufu juu ya msaada huu apewe Mungu, maana hata mwandamu amewezeshwa na Mungu, hivyo atambariki na kumzidishia alipotoa kama Luka 6.38 isemavyo. Niseme! wafungwa wamefurahi, wanashukuuru sana, na mnaisaidia Serikali.

Kwa upande wao Wafungwa wa dini zote baada ya kushereheshwa na Mapochopocho ya Mkristo huyo, Manyapara wa Gereza Wanaume na Wanawake walimuomba Mkristo huyo afike Isanga, ili wampe Shukurani toka kwa Wafungwa, ambapo alitembezwa maeneo waliyopo Sambamba na Mchungaji, Rouden Mgoje Ananyisye, kwa niaba ya Askofu Kinyunyu.

“Tunakushukuru kwa kuona umuhimu kwamba hata sisi tunatakiwa kushrehekea Krismas kwa Kula na Kunywa kama watu wengine walioko majumbani mwao ili kukumbuka kuzaliwa kwa Mkombozi ‘Yesu Kristo’ ili tukombolewe katika Maisha haya.

“Kwaa Niaba ya Wafungwa wenzengu wa Gereza la Wanaume, tunakushukuru kwa Ukarimu ambao ulifanywa pia na Mamajusi, pale walipomtembelea Mtoto Yesu akiwa amelala kwenye ‘Hori la Kulia Ng’ombe’ na Nyapara wa Kike akaongeza, “Mungu akubariki sana, walisema Nyapara hao ambao majina yamehifadhiwa.

Akijibu Shukurani hizo, Mkristo huyo alinukuu Biblia katika Yohana 8:4-7; Kisha wakamwuliza Yesu, "Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi. Katika Sheria yetu Mose alituamuru mwanamke kama huyu apigwe mawe. Basi, wewe wasemaje?"

Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole. Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, "Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe." Akasema hata yeye hawahukumu, Ila wasitende dhambi tena.

No comments:

Post a Comment

Pages