Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

DAKTARI ZANZIBAR MATATANI KWA KUMKASHIFU MTUME MUHAMMAD 'S.A.W'

Na Talib Ussi, Zanzibar

Baraza la Madaktari Zanzibar limemsimamisha kazi Dk. Abdallah Saleh Abdallah kwa muda wa miezi mitatu ili kupisha uchunguzi dhidi ya madai yake ya kumkashifu Mtume Muhammad (S.A.W) wiki iliyopita.

Haya yalibainishwa na mwenyekiti wa Baraza hilo Dk. Jamal Adam Taib wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa na kuleeza kuwa kitendo alicho kifanya Dk. Huyo kiliwaumiza wengi kwa hiyo wanataka na Bazara lijiridhishe.

“Taratibu za uchunguzi wa kosa lake zinaendelea na Baraza ili waweze kumchukulia hatua za kisheria zinazostahiki” alieelza Mwenyekiti huyo.

Awali Dk. Abdallah alikua anafanyakazi katika kitengo cha wazazi katika Hospital ya Mnazi Mmoja Zanzibar kabla ya kuhamishiwa Hospital ya Wete kisiwani Pemba .

“Baraza letu lilipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za daktar huyu na sasa tumekutana na wajumbe wote na tumeaamua apishe uchunguzi ufanye kazi” alifahamisha Mwenyekiti ambaye ni Dk. Taib.

Dk. Taib alieleza kuwa kwa mujibu wa sheria 1969 na 12 kifungu 18 (2) inapotokea mamlaka kumsimamisha muhusika baraza inatakiwa kuunda timu ya kufanya uchunguzi dhidi ya mshukiwa kwa lengo la kugundua iwapo ana hatia au hana.

“Tunachokifanya kila mmoja apate nafasi ya kujieleza baada ya hapo ndio tutaweza kutoa maamuzi lakini kitendo kilichofanyika kimetufadhaisha sanaa na tunaahidi tutalishuhulikia kwa nguvu zote” alieelza Dr. Taib.

Dr. Abdallah alifika Nchini akitokea Romania ambako ndiko aliokpata elimu yake ya udaktari na baadae kuhamia uengereza na alipofika Zanzibar aliomba usajili na kwa mujibu wav yeti alikubaliwa

No comments:

Post a Comment