HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 30, 2016

Vitendo vya ubakaji, ulawiti vyakithiri

NA TATU MOHAMED

WAKATI taarifa za Jeshi la Polisi zikionyesha kupungua kwa baadhi ya matukio ya uhalifu kwa mwaka 2016 unaoishia matukio ya ubakaji na ulawiti yameonekana kuzidi kushamiri na kuongezeka katika jamii.

Hayo yameelezwa na Jeshi la polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwamba, matumio ya ubakaji yamengezeka kwa asilimia 6 huku ulawiti ukiongezeka kwa asilimia 23.5.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kwa mwaka 2015, matukio ya ubakaji yalikuwa 927 na mwaka huu ni 1030.
Alisema hilo ni sawa na ongezeko la matukio 58 huku takwimu za ulawiti kwa mwaka 2015 zilionesha matumio yalikuwa 310 na mwaka huu ni 383, ikiwa ni ongezeko la matukio 73.

“Sababu za kuongezeka ama kupungua kwa matukio haya, kumetokana na juhudi za Polisi Kanda Maalum kuzuia na kupambana na uhalifu kwa kufanya doria na misako iliyopelekea kukamatwa kwa wahalifu kwa kushirikiana na raia wema kwa kutupatia taarifa za siri ili kugundua makosa ambayo yanakera jamii,” alisema.

Kwa upande wa matukio yaliyopungua, ni mauaji kutoka 327 hadi 291, wizi wa watoto 26 hadi 19, kutupa watoto 27 hadi 15, unyang’anyi wa kutumia silaha 204 hadi 127, unyang’anyi wa kutumia nguvu 1181 hadi 874.

Mengine ni uvunjaji 5677 hadi 5355, wizi wa magari 392 hadi 321, wizi wa pikipiki 2644 hadi 2191 na wizi wa mifugo 197 hadi 163.

Sirro alisema idadi ya watuhumiwa 7625 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kupatikana na bhangi, 269 kwa makosa ya Madawa ya kulenya aina mbalimbali, 52 kwa makosa ya ujambazi ambapo jumla ya silaha 67 na risasi 1076 za aina mbalimbali zilikamatwa pamoja na wahamiaji haramu 105 toka mataifa mbalimbali.
“Jumla ya wahalifu wote ni 13,626…..

Operesheni zilifanyika kwa kutumia vikosi mbalimbali vya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, likiwemo kikosi maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha, kikosi cha Mbwa na Farasi, Kikosi cha kuzuia wizi wa Magari, kikosi cha Askari Kanzu, Kikosi cha Interejensia pamoja na Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) zimeweza kuleta mafanikio mbalimbali,” alisema.

Pia, Sirro alisema Desemba 21 mwaka huu saa 5:00 mchana maeneo ya Tabata Bima, Jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wanne wakiwa na gari moja aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 188 CZN nyeupe lililoibiwa mkoani Kilimanjaro, watuhumiwa walitumia ufungua bandia.

Aidha, Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani limefanikiwa kukusanya jumla ya sh. 565,410,000 kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla alisema kwa jitihada za kudhibiti na kukomesha uingizwaji wa bidhaa za magendo nchini, wamefanikiwa kukamata bidhaa za magendo zenye thamani ya sh. 4,016,213,034.23 zenye kodi kiasi cha sh. 3,275,981,395.93 katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizitaja baadhi ya bidhaa zilizokamatwa kuwa ni magari 249, pikipiki 48, mafuta ya kula lita 473.620, sukari kilo 12150, mchele kilo 2,650 pamoja na majahazi matano.
“Kufanikiwa kwa zoezi la doria kudhibiti bidhaa za magendo kunatokana na ushirikiano kati ya TRA, TPDF,TISS,TPF, Jeshi la Polisi na matumizi ya vifaa vya teknolojia ya hali ya juu na taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Aliyataja baadhi ya maeneo yanayoongoza kwa kuingiza bidhaa za magendo kuwa ni Bagamoyo, Saadani, Mlingotini, Ufukwe wa Bamba, Pemba Mnazi, Kibada, Nyamisati, Msasani, Mkuranga, Ubungo, Mbweni, Kisiju, Ununio, Kunduchi, Kawe pamoja na Kigamboni.

No comments:

Post a Comment

Pages