HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2016

WAKULIMA WA KOROSHO TANDAHIMBA WAULALAMIKIA UONGOZI WA AMCOS

BAADHI ya wakulima wa korosho waliopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wameulalamikia uogozi wa Chama cha ushirika cha Amcos kwa kutowalipa fedha za korosho zao kwa zaidi ya miezi mitatu sasa tangu walipozichukua na kwenda kuziuza mnadani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakulima hao walisema kutopewa fedha na chama hicho ambacho kiliuza mazoa yao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kumesababisha maisha yao kuwa magumu.

Mmoja wa wakulima hao Buhani Hamdani alisema  tangu Oktoba 15 mwaka huu wameuza mazao yao kwa chama hicho na vingine lakini hadi sasa hakuna fedha yoyote waliokwisha pewa.

Alisema wamekwisha jaribu kuwauliza viogozi wa chama hicho kuwa ni nini tatizo lakini wameambiwa  hesabu za malipo yao bado hazijakamilika hivyo wanapaswa kusubiri.

“Mazao yetu yamekusanywa muda sana na tunajua wameshayauza sasa watuambie tatizo ambalo linawafanya mpaka leo wawe bado awajatulipa, kiukweli maisha yamekuwa magumu sana kwetu tunatakiwa kuwasomesha watoto lakini tunashindwa kutokana fedha hakuna tukiuliza tunaambiwa tusubiri mahesabu bado hayajakamilika,”alisema.

Aidha Hamdani alisema cha kushangaza vyama cha ushirika vimeanza kuwalipa watu wachache fedha zao ambao waliuza mazao yao mwezi huu lakini kwa mnada wa bei ya chini huku wale wa zamani wakiambulia patupu.

“Baada ya kulalamika sana vyama zimeanza kuwalipa watu wachache fedha zao lakini wakulima hao ni wale waliouza mazao yao mwezi huu ila wale wazamani wengine wamelipwa kidogo sana wengine kama sisi hatujaambulia kitu,” alisema.

Naye Juma Mussa alisema hali iliyopo sasa inatisha kwani hawana fedha na maisha yanazidi kuwa magumu kwao hivyo wanaiomba serikali kuingilia kati jambo hilo.

Kiongozi wa Chama cha Ushirika cha Amcos, Rajabu Timane alisema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi wakati wa mauzo kwani wanaweza kuuza lakini wakienda benki hawakuti fedha.

Alisema yeye ana gari tatu zilizokuwa na mazao na tayari yameshauzika lakini fedha zake kwenye akaunti hakuna hivyo amechukua hatua ya kuwaambia wahusika wa benki na wanalifanyia kazi jambo hilo.

“Unajua sisi tukishauza mazao fedha zinapelekwa benki sasa unapokwenda huko unakuta vitu vimepisha au hakuna fedha unafanyaje, jukumu kubwa tunawaeleza wahusika kisha wanalifanyia kazi, na nikwambie ndugu mwandishi sijawahi kuwalipa wakulima hao chini ya Sh. 3895,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages