HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2016

WAZIRI MAHIGA APOKEA MSAADA WA SHS. MILION 108

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imepokea msaada wa Milioni 108 kutoka serikali ya Korea kwa ajili ya kusaidia wahanga wa maafa ya tetemeko la Ardhi yaliyotokea Kagera Septemba, mwaka huu.

Akipokea hundi ya msaada huo  jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alisema umetolewa kusaidia kukarabati miundombinu, makazi ya watu , Shule pamoja na waathirika wote.

“Huu ni mchango mkubwa  ingawa umekuja miezi michache baada ya matokeo, lakini nyinyi wenyewe mmeshuhudia kwamba bado kazi ni kubwa ya kuweza kurekebisha miundombinu, makazi ya watu, shule pamoja na mahitaji mengine,” alisema.

Alisema Korea ni Nchi ambayo imejenga  uhusiano mkubwa  na Tanzania,  ambapo ni miaka 25 tangu ianzishe Ubalozi wake hapa Nchini, na wiki  Raisi wiki iliyopita Rais John Magufuli amesema serikali imejipanga kujenga ubalozi wake nchini humo mapema mwakani.

“Korea imeamua kwamba katika ushirikiano wa maendeleo na Nchi za kiafrika, Tanzania itapewa kipaumbele nafasi ya kwanza na nchi ya nane duniani….mwezi uliopita tulikuwa Addis Ababa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea nilikutana nae akatupa tangazo hilo na ndipo alipotoa msaaada huu tulioupokea,” alisema na kuongeza kuwa:

“Wakorea wanatusaidia sana katika uwekezaji wakiuchumi, ustawi wa jamii, wanajenga hospitali ya Mlongazira na Chanika, wametoa milioni 100 kwa ajili ya ujenzi huo lakini pia wanadhamiria kujenga daraja la kisasa katika eneo la Salenda mapema mwezi ujao,” alisema.

Mbali na hayo alisema, pia kutakuwa na uwekezaji wa aina mbalimbali kutoka kwa wakorea ambapo  katika sekta ya Kilimo, Viwanda, Utalii na pia wako tayari kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa vijana pamoja na kutoa msaada kwa chuo cha diplomasia kilichopo Kurasini, jijini Dar es Salaam.

“Kwa leo ni sherehe fupi lakini ina uzito mkubwa, mimi nimepokea hundi hii kwa niaba ya Waziri Mkuu, na wakorea wametuhakikishia kwamba urafiki wao utaendelea, na ni matarajio yao kwamba hivi karibuni wakuu wao wa Korea hasa lile Shirika lao la Maendeleo la Konica watakuja mwezi Machi katika ufunguzi wa Hospitali ya Mlongazira na Chanika,” alisema Mahiga.

No comments:

Post a Comment

Pages