HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2017

ACT-WAZALENDO: WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WAACHWE KATIKA MAENEO YAO.

NA SAID POWA, GEITA

ALIYEKUWA mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Chama hicho, Anna Mghwira, ameitaka serikali kuwaacha wachimbaji wadogo wa madini kwenye maeneo yao badala ya kuwaondoa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa ufunuzi wa Kampeni za Udiwani katika Kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome mkoani Geita.

Mghwira alisema mkoa wa Geita umejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za madini lakini wananchi wa mkoa huo wamekuwa wakiishi katika maisha duni.

"Ndugu zangu wa Nkome mnaona hali zenu zilivyo, si kwa sababu hamna rasilima ila, rasilimali zenu mmenyimwa fursa ya kuzichimba," alisema.

Aidha alifafanua kuwa kitendo cha serikali kugawa maeneo kwa wawekezaji kutoka nje na kuwanyima fursa wananchi ambao ndio wenye asili ya maeneo hayo.

Nae mgombea wa udiwani katika kata hiyo, Kulwa Kalukole, aliwaambia wananchi waliofika kwenye mkutano huo kuwa anatambua changamoto zinazo wakabili na yuko tayari kupambana nazo.

Akizitaja changamoto hizo, Kalukole alisema kumekuwa na matatizo ya maji safi na salama, barabara mbovu, umeme pamoja na kutofikishwa kwa walengwa asilimia tano ya fedha za Mapato ya Halmashauri kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Mgombea huyo alisema kumejitokeza tatizo la utoaji rushwa kwa baadhi ya wagombea na kumtaka msimamizi wa uchaguzi huo kufuatilia kwa karibu, baadhi ya wagombea wanaoshirikiana na viongoziwa vyama vyao.

"Kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa rushwa kwa wapiga kura ikiwamo rushwa ya kutoa huduma ya usafiri wa bure kutoka katika kata hiyo na kwenda Geita mjini.

Kwanini hili linajitokeza wakati huu wa uchaguzi na sio kipindi kingine!," Alihoji mgombea huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages