HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2017

AJIM yatoa mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio kituo cha kulelea watoto cha Nuru Orphans

NA KENEETH NGELESI, MBEYA

UONGOZI wa kampuni ya AJIM ENTERPISES limited ya jijini Mbeya ameahidi kutoa msaada wa mifiko 20 ya saruji kama kianzio kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha kulelea watoto yatima na waliotelekezwa na wazazi wao cha ‘NURU ORPHANS CENTER’ kilichopo Uyole Nje kidogo ya jiji  la  Mbeya.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo James Mwampondele kituo hapo  mara baada ya kukabidhi  msaada wa chakula,Mbuzi  kwa ajili ya watoto, alisema kuwa ameamua kutoa msaada
huo wa saruji ili kuanza ujenzi wa uzio ili kuweza kuwaweka maali salama watoto wanao lelewa kituoni hapo.

Awali akingumza changamoto  za kituo hicho Mkurugenzi wa kituo Jason Mark Fihavango alisema kuwa  kituo hicho kinakabiliwa na changamoto lakini kubwa zaidi ni usalama wa watoto ambao kuanzia mwaka 0-10 .

Kukosekana kwa uzio ni changamoto kubwa na kwamba walifanya upembuzi na kubaini kuwa jumla ya shilingi milioni 100 zinahitaji ili kukamilisha ujenzi lakini kazi hiyo imekwama kutokana ukosefu wa fedha.

Kutokana na kilio hicho Mkurugenzi wa Ajim, Mwapondele aliahidi kutoa msaada wa mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kunza ujenzi huku akiwa taka wadau kuguswa na tatizo hilo  huku akimtaka mkurugenzi huyo kuanza Ujenzi kwa kutumia kiasi kidogo kilichoto.

‘ Mimi niwapongeze kwa juhudi mnazo fanya za kulea watoto hao lakini nimeguswa na hili suala la uzio, naomba nitoe
mifuko 20 ya saruji lakini pia nishauri muanze ujenzi  wa msingi alafu badaye ukuta watu wakiona mmeanza wataguswa tu’ alisema Mwapondele

Aidha katika hatua nyingine Mwapondele alisema watoto wanatoka katika vituo huo wamekuwa wakikabiliwa na matatizo Lukuka likiwepo la kukosa mikpo ya elimu ya juu hivyo aliisahuriu Serikali kuwasomeshe bure kuanzia kidato cha  kidato cha tano na cha sita lakini pia wapewe upendeleoa wa mikopo wanapofika vyuo vikuu bila kujali wanacho
kisomea, kwani vituo hivi huwa vinashindwa kumudu gharama hizi.

Mbali hilo lakini pia ameomba Serikali kutoe upendeleo wa kimatibabu kwa watoto katika hospitali za serikali  huku akiwapongeza watu waliofungua vituo hivi kwa moyo wa kujitoa kataka kufanya kazi ya kuwalea watoto wenye mahitaji maalumu.

Naye Mkurugenzi wa kituo hicho Fihavango aliipongeza kampuni hiyo kwa kukitembelea kituo hicho na kula chakula pamoja pamoja huku akiitaka jamii kuiga mfano wa kamapuni ya Ajim kwa kutoa msaada chakula lakini
pia kugushwa na tatizo la uzio hali iliyo mlazimu Mkurugenzi kutoa saruji.

‘Nina watoto zaidi ya 20 wenye kunazi miaka 0-10 hivyo changamoto hazikosekana katika masuala ya mavazi kwani kuna wengine wanasoma lakini changamoto kubwa zaidi ambalo ningeomba wadau watakao guswa kama Ajim ni uzio kwani tulifanya fanya upembuzi tunahitaji shilingi
milioni 100 ili kikamilisha kila kitu’ alisema Fihavango

No comments:

Post a Comment

Pages