Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

BOTI YAUA 12 YAJERUI 27

NA MBARUKU YUSUPH, TANGA

WATU 12 wamepoteza maisha baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kuzama huku wengine 27 wakijeruhiwa.
Jahazi hilo linalofanya safari zake kati ya Pemba na Tanga lilizama katika kisiwa cha Jambe kilichopo bahari ya Hindi nje kidogo ya jiji la Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ilitokea saa 12:30.

Wakulyamba alisema jahazi hilo lilikuwa linaendeshwa na nahodha Badru Sa.idi, ambaye pia alifariki lilikuwa na namba za usajili MV Z5512 maarufu kama Sayari
Alisema juhudi za kuopoa miili inaendelea.

Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na Jeshi la Polisi linachunguza ili kubaini huku taarifa za awali zikisema kuwa chombo hicho kilipigwa wimbi eneo la nyuma na kupoteza muelekeo.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk. Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea miili 12 pamoja na majeruhi 25.

Aidha alisema kuwa kati ya maiti hizo sita ni watu wazima na sita ni watoto wadogo ambao bado hawajatambuliwa na imehifadhiwa hospitalini hapo.
Baadhi ya majeruhi walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali.

Juma Maduhu Mkazi wa Bariadi alisema kuwa chombo hicho kiliondoka saa 4:00 usiku na baada ya mwendo wa masaa mawili nahodha alilazimika kusimamisha safari kutoka na kuwepo na upepo mkali baharini.

Alisema kuwa walipofika katika kisiwa cha Jambe jahazi hilo lilianza kujaa maji ndani na kuanza kutoa ambapo yaliwashinda nguvu na kusababisha chombo hicho kupasuka na kuzama.

Mbunge wa Tanga (CUF), Mussa Mbaruku, ametoa msaada wa sanda kwa maiti 12 na kuwataka wafiwa kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki cha msiba.

Mbunge huyo aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa boti lililoletwa kwaajili ya Bagamoyo kwenda Dar es Salaam kuhamishiwa Tanga.

No comments:

Post a Comment