HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 02, 2017

'CCM haina uwezo wa kuzuia mabadiliko'

Na Talib Ussi, Zanzibar

Mwanasheria Mkuu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Othman Masoud Othman amesema kuwa chama cha Mapinduzi kimeshuka kiushindani Visiwani humu na kueleza kuwa hakina tena uwezo kuzuia mabadiliko.

Othman aliyaeleza hayo katika Kongamano la liloandaliwa na wanafunzi wa vyuo Vikuu ambao wanaiunga mkono chama cha Wananchi (CUF) huko Mazson Hotel Mjini hapa.

Alieelza kuna ushahidi uliowazi kwa chama hicho kwa hakina tena nguvu ya kushindana chama chochote kile kutokana viongozi wake kuwa hawana tena uwezo wa kuwashawishi wananchi kinyuume ilivyokua na chama cha  Afro Shirazi Part (ASP).

Alieleza katika mwaka 1961 Zanzibar ilifanya uchaguzi ambapo chama cha ASP kilipata ushindi wa 7% lakini alieleza kuwa kutoka na Viongozi wake kuwa na nguvu ya ushawishi baada ya miaka Miwili ulifanyika uchaguzi tenna ambapo kwa Pemba 1963 waliweza kupata kura 44.7%.

“Sasa lakini vijana hemu angalieni leo Uchaguzi wa 1995 CCM ilipata kura karibuni 20000 kutoka Pemba lakini mwaka 2000 walipa kura 10000 na hata mwaka juzi  sijui kuwa walifika hata 7000 kutoka Pemba hii ni kuonesha kuwa hawana tena nafasi ya kushika dola katika Visiwa hivi vya Zanzibar” alieelza Mwanasheria huyo ambaye alifukuzwa baada ya kupingana na CCM katika Bunge la Katiba.

Kutokana na hayo Othman aliwataka vijana kuisoma historia ya Nchi yao ili waweze kuwa na uzalendo uliotukuka.
Sambamba na hilo kuhusu kile kinachodaiwa na CUF kuporwa haki yao katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2015, aliwaambia vijana wasiwe na ghofu hata kidogo walishaimaliza tokea kwenye uchaguzi huo sasa imebakia siku na saa tuu kurudi kwa haki yao.

“Mkiona gogo mlilolikata bado lipo juu si kwa sababu halijakatika bali kuna miti imelishika lakini ukweli limeshakatika na litaanguka tena katika kipindi kifupi mnoo” alieeleza Nguli huyo wa Sheria.

Alifahamisha kuwa kazi ya wananchi ilishamaliza tangu mwaka Juzi October na kudai kilichobakia ni kazi ya  Viongizi wao na Dunia kufanya juhudi ambayo alieelza kuwa ambayo imefanywa kwa hatua kubwa na matunda yake alidai yataonekana hivi karibuni.

“Ukweli ukisimama hakuana ambacho kitazuia haki isionekane” alifahamisha Othman.
Alieelza kuwa kilichobakia kwa viongozi waliopora haki ya wazanzibar kazi ya ni kutisha watu kwa kuwapiga na kuwavimia kwa mapanga.

“Ukimuona mtu mzimaa anapigana na mtoto huku kashika Panga ujue keshazidiwa, Vijana ondoeni ghofu mabadiliko ya kazi mlioifanya yameshaanza kuonekana” alieelza Othman.
Kauli hiyo inavunja maneno ya katibu mwenezi wa CCM Hamphrey Pole Pole ambaye alisikia katika masuku ya hivi karibuni akisema kuwa chama chake kiko imara na kazi kubwa iliyombele yao ni kuwadhibiti wanachama wake ambao hawakubaliani na maamuzi ya chama chao.

Profesa Abdulkadir Shariff alieleza kuwa mateso wanayoyapata wakaazi wa Zanzibar hasa katika Kisiwa cha Pemba hawawezi hata siku moja kikiunga mkono chama tawala.

“Umpe mtu kila aina ya mateso halafu ufikirie siku ya siku watakuja kukupigia kuraa, hapana na hili walilolifanya watawala ndio limekuwa adhabu kwao” alieleza Pr. Sheriff.
Nao wanafunzi waliondaa Kongamano hilo walisema muda umefika sasa kwa wasomi kutoa taaluma ambayo itawawezesha wazznzibar kuitambua Nchi yao ambayo itawapa kuwa na mapenzi nayo na hatmae kuleta umoja na upendo

No comments:

Post a Comment

Pages